We Like Sharing

Wednesday, January 25, 2017

Wauza mkaa waua mlinzi wa misitu, Nzega mkoani Tabora

Wauza mkaa waua mlinzi wa misitu, Nzega mkoani Tabora

Wauza mkaa waua mlinzi wa misitu, Nzega mkoani Tabora

Nzega, Tabora

Kijana mmoja mkazi wa mjini Nzega, mkoani Tabora ambaye hujishughulisha na ulinzi wa misitu wilayani Nzega amepoteza maisha baada ya kuzidiwa nguvu na kikundi cha wauza mkaa waliokuwa wakisafirisha mkaa kuelekea Shinyanga.

Tukio la mauaji ya mlinzi huyo limetokeo alfajiri ya kuamkia leo tarehe 24/1/2017 katika maeneo ya Mnadani, magharibi mwa mji wa Nzega, alipokuwa katika lindo la kudhibiti wafanyabiashara wa mkaa wanaosafirisha mkaa kutoka Tabora kwenda Shinyanga, ambapo askari huyo akiwa na mlinzi mwenzake (hajafahamika), walifanikiwa kuzuia msafara wa wauza mkaa hao lakini kwa bahati mbaya walinzi hao walizidiwa nguvu hivyo mmoja akafanikiwa kukimbia, huku mwenzake akipoteza maisha kwa kuchinjwa.

Hata hivyo, taarifa zinasema kuwa ofisi ya Misitu wilayani humo imekanusha kuwa haikuwa na taarifa za mlinzi huyo kuwa lindoni.

Mkuu wa wilaya ya Nzega, Bw. Godfrey Ngupula amethibitisha kutokea kwa tukio la mauaji hayo ya kinyama na amesikitishwa na tukio hilo. Akizungumza na wakazi wa mji wa Nzega, mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo la wafanyabiashara wa mkaa kusitisha mara moja biashara hiyo, kwani inachangia kwa asilimia kubwa katika uharibifu wa mazingira na kupelekea wilaya hiyo kuwa Jangwa.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Nzega mjini, kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Bw. Hussein Mohamed Bashe amesema biashara ya mkaa inagusa uchumi pamoja na maisha ya watu kwa ujumla kwa maana kwamba watu wanahitaji mkaa kama nishati kwa matumizi majumbani. Halikadhalika kuna watu wanaendesha maisha yao kwa kutegemea biashara ya mkaa hivyo biashara ya mkaa haitakiwi kukomeshwa ghafla ili wananchi wanaoendesha maisha yao kupitia biashara hiyo wasipate taabu.

Mbunge huyo, ambaye ametimiza mwaka mmoja tangu aingie madarakani, amemshauri mkuu wa wilaya ya Nzega kuzishauri TC DC na Idara ya Maliasili kukaa meza moja na kufanya yafuatayo.

  1. Kujua mahitaji sahihi ya mkaa kwa mwaka wilayani humo ili kubaini kiwango cha miti itakayotumika.
  2. Kusajili wauzaji na wachoma mkaa wa vijijini ili watambulike na kuwataka kupanda miti katika maeneo wanayovuna miti hiyo na kujua ukomo wa uzalishaji
  3. Kutambua vijiji vinavyozunguka mapori ya hifadhi ya misitu na kuwafanya wananchi waishio katika vijiji hivyo kunufaika na uwepo wa misitu hiyo katika maeneo hayo.
  4. Kuzuia uzalishaji na uuzaji wa mkaa nje ya wilaya ya Nzega. Mkaa utakaozalishwa utumike Nzega pekee.
  5. Kuanzisha programu ya kutumia Takangumu na majani ya mpunga kuzalisha mkaa

Biashara ya mkaa imekuwa ikifanyika mkoani Tabora kwa muda mrefu sana na imekuwa mkombozi kwa watu wasio na uwezo wa kiuchumi. Wafanyabiashara wa mkaa hununua mkaa unaozalishwa katika maeneo ya hifadhi ya misitu na kisha kuusafirisha mkoani Shinyanga wanakouuza kwa bei ya juu, hali inayosaidia kukuza vipato vyao.

Serikali imekuwa ikipambana na wauzaji hao wa mkaa kwa kipindi kirefu kiasi kwamba umetengenezeka uhasama baina ya wafanyabiashara hao na maafisa misitu au walinzi wa misitu. Mara nyingi walinzi wamekuwa wakiwakamata wafanyabiashara na kuwanyang'anya mkaa na vyombo vyao vya usafiri (baiskali).

Zinazofanana na hii

Mkoa wa Tabora
Wilaya ya Nzega
Wilaya ya Tabora
Wilaya ya Igunga
Wilaya ya Urambo
Maofisa wa mbunge, wataalam wa maji na wenyeviti wa mitaa mjini Nzega wafanya kikao
Mjue Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Mohamed Bashe
Wauza mkaa waua mlinzi wa misitu, Nzega mkoani Tabora

Wengine wanasoma hizi:

Jinsi ya kuweka screen lock kwenye android

Kampuni kubwa zinazotengeneza Smartphones

Rais mteule wa Gambia, aapishwa nje ya nchi

Mambo ya kufanya baada ya kununua smartphone

Habari za michezo

Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017

Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC

Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup

Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe

Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment