We Like Sharing

Wednesday, November 30, 2016

Mkoa wa Tabora

Mkoa wa Tabora

Mkoa wa Tabora

Tabora, Tanzania

Ramani ya mkoa wa Tabora ikionesha wilaya zote za mkoa huo
Tabora ni miongoni mwa mikoa 30 ya Tanzania. Mkoa huu upo magharibi mwa nchi na unapakana na mkoa wa Kigoma kwa upande wa magharibi, Shinyanga kwa upande wa kaskazini, Singida upande wa mashariki, Rukwa upande wa kusini magharibi pamoja na mbeya kwa upande wa kusini.

Mkoa huu una eneo lenye ukubwa wa kilometa za mraba 76,151, ambapo 46% ya eneo hilo ni hifadhi ya misitu na 22% ni hifadhi ya wanyama. Ardhi ya mkoa huu ina rutuba inayofaa kwa kilimo cha mazao ya aina mbalimbali. Mji mkuu wa mkoa huu unaitwa Tabora na upo katikati ya wilaya zote za mkoa wa Tabora.

Mkoa wa Tabora kwa sasa una jumla ya wilaya saba, ambazo ni Nzega, Igunga, Uyui, Sikonge, Urambo, Kaliua pamoja na Tabora (manispaa). Wilaya ya Kaliua ilianzishwa mwaka 2012. Kabla ya uanzishwaji wa wilaya ya Kaliua mkoa wa Tabora ulikuwa na jumla ya wilaya sita.

Wenyeji wa mkoa huu ni wanyamwezi. Pia kuna makabila mengine ambayo ni pamoja na wasukuma, waha, wanyakyusa, wachagga, waarabu, n.k. Asilimia kubwa ya wakazi wa mkoa huu wanajishughulisha na kilimo na ufugaji.

Mazao yanayozalishwa zaidi katika mkoa huu ni pamoja na Tumbaku, Mpunga, viazi vitamu, Mahindi, Mtama, Pamba, alizeti na karanga. Pia mkoa huu unasifika zaidi kwa ufugaji wa nyuki na unazalisha asali nyingi sana inayouzwa ndani na nje Tanzania.

Kwa upande wa usafiri na mawasiliano, mkoa huu kwa miaka kadhaa nyuma ulikuwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa barabara za lami, lakini siku za hivi karibuni serikali imefanikiwa kujenga barabara ya Tabora mjini - Nzega kwa kiwango cha lami, pamoja na zile zinazounganisha mikoa jirani. Pia barabara nyingi za Tabora mjini na baadhi ya halmashauri za wilaya zimeshawekewa lami.

Mkoa huu una vituo viwili (2) vya Redio (kwa sasa) ambavyo ni CG FM pamoja na Voice of Tabora (V.O.T) na kwa kiasi fulani vinasaidia kutoa taarifa za ndani ya mkoa kwa wakazi wa mkoa wa Tabora na baadhi ya mikoa jirani.

Tofauti na miaka ya zamani, ambapo watu walikuwa wanautambua mkoa wa Tabora kuwa ni mkoa mchafu wenye nyumba za kizamani, kwa sasa hali ni tofauti kabisa, kwani nyumba nyingi nzuri na za kisasa zimejengwa miaka ya hivi karibuni na watu wanazidi kujenga nyumba nyingi za kisasa, hivyo kuifanya miji ya mkoa huu kuwa na muonekano wa kisasa zaidi hususani Manispaa ya Tabora na Nzega.

Wakazi wa mkoa huu wanasumbuliwa na changamoto ya uhaba wa maji hususan wakati wa kiangazi, lakini habari njema ni kwamba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshaahidi utekelezaji wa ujenzi wa bomba litakaloleta maji mkoani tabora kutoka Ziwa Victoria utaanza mwanzoni mwa mwaka ujao (2017). Mradi huo utafuta kabisa tatizo la uhaba wa maji kwa wakazi wa mkoa wa Tabora.

Wafuatao ni wabunge wanaopambana kwa kadri ya uwezo wao kwa ajili ya kuuletea maendeleo mkoa wa Tabora. Kwenye mabano ni majina ya majimbo wanayosimamia:

  • Husseina Mohamed Bashe, CCM (Nzega Mjini)
  • Dr. Hamisi Andrea Kigwangalla, CCM (Nzega Vijijini)
  • Selemani Zedi, CCM (Bukene)
  • Ntimizi Rashid Mussa, CCM
  • Dr. Dalaly Peter Kafumu, CCM (Igunga)
  • Magdalena Sakaya, CUF (Kaliua)
  • Seif Hamis Said Gulamali, CCM (Manonga)
  • George Kakunda, CCM (Sikonge)
  • Emmanuel Mwakasaka, CCM (Tabora Mjini)
  • John Peter Kadutu, CCM (Ulyankulu)
  • Margareth Sitta, CCM (Urambo)
  • Maige Athumani Almasi, CCM (Uyui)
Zinazosomwa zaidi
Ramani ya Tanzania ikionyesha mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani

Zinazofanana na hii

Wilaya ya Nzega
Wilaya ya Tabora
Wilaya ya Igunga
Wilaya ya Urambo
Maofisa wa mbunge, wataalam wa maji na wenyeviti wa mitaa mjini Nzega wafanya kikao
Mjue Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Mohamed Bashe
Wauza mkaa waua mlinzi wa misitu, Nzega mkoani Tabora

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment