Wilaya ya Tabora
Tabora, TanzaniaWilaya ya Tabora ni miongoni mwa wilaya 7 zinazounda mkoa wa Tabora. Wilaya hii pia ndio makao makuu ya mkoa na Manispaa ya Tabora. Wilaya hii inapakana na wilaya ya Uyui kwa upande wa kaskazini, mashariki na Magharibi. Upande wa kusini inapakana na wilaya ya Sikonge.
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Manispaa ya Tabora ina jumla ya wakazi 226,999. Wanaume ni 111,361 na wanawake ni 115,638. Wenyeji wa wilaya hii ni wanyamwezi kama ilivyo kwa wilaya nyingine za mkoa wa Tabora. Pia kuna makabila mengine kama vile wasukuma, waha, waarabu, na wanyaturu.
Shughuli kubwa zinazofanywa na wakazi wa wilaya/manispaa ya Tabora ni kilimo, ufugaji pamoja na biashara. Mazao yanayozalishwa katika wilaya hii ni pamoja na Tumbaku, Pamba, alizeti, mahindi, mpunga na mtama. Wakazi wa wilaya hii pia wanajishughulisha na ufugaji wa nyuki wa asali.
Reli ya kati inapita katikati ya mji wa Tabora, makao makuu ya wilaya ya Tabora. Pia miundombinu za barabara zinazounganisha wilaya hiyo na wilaya nyingine za Tabora zinazidi kuboreshwa ikiwa ni pamoja na kujengwa kwa kiwango cha lami. Serikali imefanyakazi kubwa ya kuziwekea lami barabara nyingi za mitaani mjini Tabora, hali inayoupa muonekano mzuri zaidi mji wa Tabora.
Manispaa ya Tabora ina Hospitali moja (1) inayomilikiwa na serikali ya mkoa. Pia ina vituo vya afya na zahanati kadhaa zinazomilikwa na halmashauri, taasisi za serikali pamoja na mashirika ya kidini.
Kwa upande wa elimu, wilaya ya Tabora ina shule za msingi na sekondari. Baadhi ya shule za sekondari maarufu mjini Tabora ni shule ya sekondari ya wavulana (Tabora Boys) pamoja na shule ya wasichana (Tabora Girls). Pia kuna vyuo vinavyotoa elimu ya kati na ya juu. Miongoni mwa vyuo hivyo ni pamoja na Chuo cha Utumishi wa Umma, Chuo cha Ardhi, Chuo cha Kilimo Tumbi pamoja na Chuo Cha Ualimu. Pia kuna vyuo vingine vidogo vidogo vya VETA.
Taarifa hii imeandaliwa na mwandishi wetu, kama ina mapungufu au makosa tujulishe
Habari zinazofanana na hii
Dr. Hamis Kigwangalla akamata shehena kubwa ya viroba vya konyagi na pombe haramu
Mjue Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Mohamed Bashe
ifahamu kiundani wilaya ya Igunga
Ufahamu mkoa wa Tabora
Wilaya ya Urambo Wilaya ya Nzega
Maofisa wa mbunge, wataalam wa maji na wenyeviti wa mitaa mjini Nzega wafanya kikao
Wauza mkaa waua mlinzi wa misitu, Nzega mkoani Tabora
Habari nyingine zaidi...
Rais Dkt John P Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali
Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii
Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA
Moto wateketeza nyumba na mali Unguja, Zanzibar
Taarifa aliyoitoa Moses Joseph Machali kuhusu kuhamia Chama Cha Mapinduzi
Moses Joseph Machali ahamia rasmi Chama cha Mapinduzi
Dr. Hamis Kigwangalla akamata shehena kubwa ya viroba vya konyagi na pombe haramu
Maofisa wa mbunge, wataalam wa maji na wenyeviti wa mitaa mjini Nzega wafanya kikao
Sikiliza ngoma kali za Mangwea
Trump azidi kutoa kali za mwaka, akataa mshahara mkubwa
Rais John Pombe Magufuli asaini sheria ya huduma za habari 2016
Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam
November 19, 2016
Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii
November 19, 2016
Dr. Shein azindua wodi ya watoto na wazazi
November 19, 2016
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA
November 20, 2016
No comments:
Post a Comment