Wilaya ya Igunga
Tabora, TanzaniaWilaya ya Igunga ni miongoni mwa wilaya zinazounda mkoa wa Tabora. Wilaya hiyo ina eneo lenye ukubwa wa kilometa za mraba 6,912, na ipo upande wa mashariki mwa mkoa huo wa Tabora. Wilaya hii inapaka na wilaya ya Iramba kwa upande wa Mashariki, Uyui kwa upande wa kusini, Kishapu kwa upande wa kaskazini na Nzega kwa upande wa magharibi.
Wilaya hii inapata mvua kwa kiwango kati ya 500mm hadi 700mm kwa mwaka na ina maeneo yenye misitu, vichaka, mbuga za malisho na maeneo ya Tambarare.
Wilaya ya Igunga ina tarafa nne ambazo ni Simbo, Igunga, Igurubi pamoja na Manonga. Pia wilaya hii ina jimbo moja tu la uchaguzi.
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, wilaya ilikuwa na jumla ya watu 399,727 (wanaume 195,607 na wanawake 204,120). Idadi ya kaya zote ni 62,427.
Wenyeji wa wilaya hii ni wanyamwezi. Makabila mengine yanayoishi wilayani hapo ni wasukuma, wanyaturu, waha, n.k.
Asilimia kubwa ya wakazi wa wilaya hii wanajishughulisha na kilimo, ufugaji na biashara. Miongoni mwa mazao yanayozalishwa ni pamoja na Mpunga, Mahindi, Mtama, Alizeti pamoja na Pamba.
Habari zinazosomwa zaidi
Ziara ya RC Paul Makonda jijini Dar yaibua makubwa
Ufahamu mkoa wa Tabora
Wilaya ya Nzega
Zinazofanana na hii
Mkoa wa TaboraWilaya ya Nzega
Wilaya ya Tabora
Wilaya ya Urambo
Maofisa wa mbunge, wataalam wa maji na wenyeviti wa mitaa mjini Nzega wafanya kikao
Mjue Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Mohamed Bashe
Wauza mkaa waua mlinzi wa misitu, Nzega mkoani Tabora
Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam
November 19, 2016
Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii
November 19, 2016
Dr. Shein azindua wodi ya watoto na wazazi
November 19, 2016
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA
November 20, 2016
No comments:
Post a Comment