We Like Sharing

Thursday, December 1, 2016

Wilaya ya Urambo

Wilaya ya Urambo

Wilaya ya Urambo

Tabora, Tanzania

Ramani ya mkoa wa Tabora ikionesha wilaya zote za mkoa huo

Wilaya ya Urambo ni miongoni mwa wilaya 7 zinazounda mkoa wa Tabora. Wilaya hiyo ipo upande wa magharibi mwa mkoa wa Tabora. Inapakana na wilaya za Uyui na Sikonge kwa Upande wa Mashariki, Mpanda kwa upande wa kusini (Mkoa wa Katavi) na inapakana na wilaya Kaliua kwa upande wa Kaskazini Magharibi.

Wilaya hii ina eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 6,110, na makao makuu ya wilaya yapo katika mji wa Urambo, umbali wa km 90 kutoka Tabora mjini. Wenyeji wa mkoa huu ni wanyamwezi. Shughuli kuu za uzalishaji mali wilayani Urambo ni Kilimo pamoja na ufugaji wa mifugo na nyuki. Mazao yanayozalishwa zaidi wilayani humo ni pamoja na Tumbaku, Mahindi, Pamba, Mtama, Mahindi pamoja na alizeti.

Wilaya hii ilimegwa kwa ajili ya kupata wilaya ya kaliua mwaka 2012. Reli itokayo tabora mjini kuelekea kigoma inapita katika wilaya ya Urambo. Sehemu ya wilaya hii ilikuwa kiini cha utemi wa Urambo ambako mtemi Mirambo alijenga milki yake.

Taarifa hii imeandaliwa na mwandishi wetu, kama ina mapungufu au makosa tujulishe

Habari zinazosomwa zaidi

Picha ikionesha jengo la CRDB Bank, mjini Urambo

Zinazofanana na hii

Mkoa wa Tabora
Wilaya ya Nzega
Wilaya ya Tabora
Wilaya ya Igunga
Maofisa wa mbunge, wataalam wa maji na wenyeviti wa mitaa mjini Nzega wafanya kikao
Mjue Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Mohamed Bashe
Wauza mkaa waua mlinzi wa misitu, Nzega mkoani Tabora

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment