Kupakua WhatsApp bure kupitia Play store
WhatsApp ni mtandao wa kijamii uliyojizolea umaarufu mkubwa zaidi duniani hususan kutokana na huduma zake za kusafirisha taarifa kuwa nzuri na za haraka zaidi.
Katika somo la leo, Nzegamedia, tumekuandalia hatua rahisi zitakazokupatia ufahamu wa kupakua na kuingiza App ya WhatsApp kwenye simu yako ya Android kupitia Google Play Store.
Kama umewahi kuingiza Apps nyingine kwenye simu kuptia Play Store, naimani kwenye kuingiza WhatsApp pia hautopata taabu kwa sababu hatua za upakuaji na uingizaji zinafanana. Fuata hatua rahisi zifuatazo na ndani ya dakika kadhaa utakuwa tayari umeshamaliza kupakua:
- Washa Mobile Data na hakikisha una kifurushi cha kutosha kuweza kupakua
- Hakikisha umeshafungua akaunti ya Google Play Store na inafanyakazi kwenye simu yako
- Fungua App ya Play Store
- Juu kwenye kisanduku cha kutafutia, andika WhatsApp Messenger
- Chagua App ya kwanza katika matokeo, lakini kabla ya kuichagua hakikisha ina nembo ya WhatsApp na jina linasomeka WhatsApp Messenger.
- Bofya Download
- Kubali sera na masharti ya utumiaji wa App kwa kubofya Accept na subiri hadi imalize kupakua
- Fungua akaunti yako ya WhatsApp na anza kuchati na marafiki zako.
Unaweza kupenda pia hizi:
WhatsApp ni nini?
Nini maana ya mtandao wa kijamii?
Google Play Store ni nini?.
Nini maana ya simu za mkononi?
More Articles
Habari za michezo
Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017
Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC
Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup
Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe
Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup
No comments:
Post a Comment