We Like Sharing

Monday, January 23, 2017

WhatsApp ni nini?

WhatsApp ni nini?

WhatsApp ni nini?

WhatsApp ni mtandao wa kijamii maarufu duniani inayowaruhusu watumiaji wake kutumiana jumbe za maandishi, sauti, picha pamoja au video pamoja na kupiga simu kwa sauti au kwa kuonana kwa kutumia intaneti.

Ili mtu aweze kutumia mtandao huu anatakiwa awe na namba ya simu ambayo itatambulika kwenye mfumo wa WhatsApp kama jina la mtumiaji (username).

Mtandao wa WhatsApp uliundwa 2009 na wastaafu waliokuwa wakifanyakazi katika kampuni ya Yahoo. Miezi kadhaa baada ya kuanzishwa kwake, watu zaidi ya 25,000 waliweza kujiunga na mtandao huu, na kadri muda ulivyosonga mbele idadi ya watumiaji ilizidi kukua.

Baada ya kuona idadi ya watumiaji wa WhatsApp inazidi kuongezeka siku hadi siku, wamiliki wake waliamua kuwatoza pesa watumiaji wa kiasi cha dola 0.99 kwa mwaka, isipokuwa mwaka wa kwanza anaojiunga mtumiaji ambapo alipewa ofa ya kutumia WhatsApp bure mwaka mzima.

Mwaka 2014 mtandao wa WhatsApp ulinunuliwa na kampuni ya facebook inayomilikiwa na Mark Zuckerberg.

Takwimu zilizotolewa januari 2015 zinaonesha kuwa idadi ya watumiaji wa mtandao huu pendwa iliongezeka hadi kufikia milioni 700. Mwezi februari 2016 watumiaji hai kwa mwezi mzima walikuwa bilioni moja (1 billion).

Kutumia WhatsApp

Ili uweze kutumia WhatsApp, unapaswa uwe na kifaa chenye uwezo wa kutumia WhatsApp hususan simu-janja (SmartPhones) au tablets pamoja na laini ya simu za mkononi.

Pia, kama tulivyotangulia kusema hapo juu, unatakiwa uwe na namba ya simu ambayo itatumika kukutofautisha wewe na watumiaji wengine kwenye mfumo wa WhatsApp. Kitu kingine cha muhimu ni uwepo wa internet, ambayo inaweza kuwa ni itaneti unayoipata kupitia laini yako ya simu, au mtandao wa bila waya (wireless Network/Wi-Fi).

Mwezi januari, 2015, WhatsApp waliboresha mtandao kwa kuwaruhusu watumiaji kutumia WhatsApp kwenye Kompyuta zao, lakini ili mtumiaji aweze kuunganisha akaunti yake kwenye kompyuta lazima akaunti yake ya WhatsApp iwe hewani kwenye smartphone au tablet yake na awe nayo karibu wakati wa kuunganisha.

Huduma muhimu kwenye WhatsApp

Mtumiaji wa whatsapp sit u ana nafasi ya kumtumia mtu mmoja mmoja meseji, bali anaweza kuunda kundi la WhatsApp, au kujiunga kwenye makundi yaliyoundwa na watumiaji wengine ili afurahie kutuma taarifa kwa watumiaji wengi zaidi kwa wakati mmoja.

Pia, kupitia WhatsApp mtumiaji anaweza kutuma mafaili yake ya aina mbalimbali yakiwemo mafaili yaliyotengezwa kwa kutumia program za Microsoft Office, HTML, PDF, n.k.

WhatsApp inampa nafasi mtumiaji ya kutuma ramani ya eneo alilopo. Halikadhalika mtumiaji wa mtandao huu anaweza kutuma namba za watu alizozihifadhi kwenye simu yake.

Vipi kuhusu ulinzi na usalama katika mtandao huu

Katika hali ya usalama kwa mtumiaji wa mtandao wa WhatsApp, wamiliki wake wamejitahidi sana kuweka ulinzi, ambao unasaidia kutokufanyiwa udukuzi kwa watumiaji kwa sababu akaunti ya mtumiaji mmoja haiwezi kutumika kwenye simu zaidi ya moja kwa wakati mmoja, na ili uweze kuitumia akaunti ya mtu lazima uwe na laini ya mtumiaji husika na iwe hewani ili uweze kupokea namba za uthibitisho (confirmation code).

Pia, mtumiaji wa mtandao huu anapaswa awe na umri wa angalau miaka 16. Hatua nyingine za kuimarisha ulinzi kwenye akaunti ya mtumiaji, zinatakiwa zifanywe na mtumiaji mwenyewe kupitia kwenye mipangilio ya Programu.

Unaweza kupenda pia hizi:

WhatsApp ni nini?
Nini maana ya mtandao wa kijamii?
Google Play Store ni nini?.
Nini maana ya simu za mkononi?
Facebook ni nini?

More Articles

Kulazimisha simu isome 3G tu

4G LTE ni nini?

3G ni nini na inafanyaje kazi?

2G ni nini na inafanyaje kazi?

Internet Configurations za Airtel

Internet Configurations za Halotel

Habari za michezo

Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017

Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC

Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup

Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe

Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment