Facebook ni nini?
Facebook ni mtandao wa kijamii unaowaruhusu watumiaji wake kuchapisha na kutumiana taarifa kwa njia ya maandishi, picha au video.
Mtandao huu pia unaruhusu watumiaji kutafuta marafiki wanaotumia mtandao huo kokote duniani kwa ajili ya kubadilishana nao mawazo juu ya maswala mbalimbali, eidha ya kibiashara, kisiasa, kidini, nk.
Mtandao huu wa Facebook ulianzishwa mnamo mwaka 2004 na mwanafunzi wa chuo kikuu cha Harvard, ajulikanaye kwa jina la Mark Zuckerberg na kipindi hicho ulikuwa unatumiwa na wanafunzi tu kwa ajili ya kujadili juu ya masomo yao, lakini baadae uliweza kukuwa zaidi na kuruhusu hata watu wa kawaida kutumia mtandao huo.
Kipindi unaanza kufanyakazi mtandao huo, ulikuwa katika lugha ya kiingereza tu, lakini kadri muda ulivyozidi kusonga, kurasa ziliweza kutafsiriwa katika lugha nyingine hivyo kuwavutia watu wengi zaidi hususan wale wasio na utaalam wa lugha ya kiingereza.
Kwa sasa mtandao huo unafanyakazi katika lugha zaidi ya 70, kikiwemo Kiswahili, ambacho ni lugha kuu ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwenye Facebook mtu anaweza kuchapisha chochote kwenye timeline yake, na watu wataona chapisho (post) hilo kupitia kwenye News feed, au moja kwa moja kwenye timeline ya mchapishaji. Kutegemeana na mvuto wa chapisho (post) marafiki wataonyesha hisia zao kwa kubofya kwenye kitufe cha Poa (Like) na kisha hutoa maoni yao ambayo kwa kitaalam yanajulikana kama Comments.
Maoni hayo yanaweza kuwa ya kufurahisha, kuhuzunisha, kuchekesha, kuudhi au kuchukiza kutegemeana na mada iliyotolewa na mchapishaji.
Kwa mfano mfuasi wa CCM akichapisha taarifa yenye kuwakera wafuasi wa vyama pinzani nchini Tanzania ataambulia maoni/comments za matusi na mashambulizi makali kutoka kwa wafuasi wa vyama pinzani, halikadhalika mfuasi wa vyama vya upinzani akiweka chapisho lenye kuwakera wafuasi wa CCM, cha moto atakiona.
Maneno hayo juu ni mfano tu wa namna marafiki wa naotumia Facebook wanavyoweza kutoa maoni kwenye machapisho. Tuendelee na mada yetu.
Mtandao wa Facebook unaongoza kwa kuwa na watumiaji wengi zaidi kuliko mitandao mingine. Mtandao huu pia umepata pingamizi nyingi sana katika bara la Asia hususan China ambapo serikali ya nchi hiyo imekataza raia wake kutumia mtandao wa Facebook kwa sababu za kiusalama. Mwanzilishi wa Facebook yupo katika mazungumzo na serikali ya china ili mtandao wake uweze kutumika nchini humo.
Mtandao wa Facebook pia una features za aina mbalimbali zinazofanyakazi tofauti tofauti, na mtu yeyote anaweza kuzitumia. Features hizo ni pamoja na:
Kurasa/Facebook Pages
Facebook inamruhusu mtu binafsi, kampuni au shirika kuunda ukurasa, utakaomuwezesha kuchapisha taarifa za aina mbalimbali kutegemeana na matakwa yake. Wengi wamezoea kuita Fan Page, ambapo wanaojiunga na kurasa hizo huitwa Fans, na wanajiunga kwa kubofya kitufe cha Poa (Like) ambacho kipo juu ya ukurasa.
Wasanii na watu wengi wenye umaarufu wana kurasa zao za Facebook wanazozitumia kushirikisha wafuasi wao juu ya shughuli zao. Watu kama Rais wa Marekani, Barack Obama, Donald trump na wengine wana fan pages zao.
Fan Pages huwapa nafasi watu maarufu, wafanyabiashara, kampuni na mashirika ya kujitangaza zaidi na kujipatia wafuasi wengi zaidi.
Makundi ya Facebook(Facebook Groups)
Ukiachilia mbali Facebook fan Page, Facebook inawaruhusu watumiaji wake kutengeneza makundi mapya pamoja na kujiunga kwenye makundi yaliyotengenezwa na watumiaji wengine. Makundi hayo hujikita katika jambo moja kuu au mchanganyiko, kwa mfano unaweza kukuta kundi linajadili siasa pekee, elimu pekee, uchumi pekee, nk.
Anayeongoza kundi huitwa Admin (Administrator) na wale wanaojiunga huitwa members (wanachama). Mtu yeyote anaweza kutengeneza kundi la Facebook almradi awe na akaunti ya Facebook inayofanyakazi.
Hitimisho
Kama hujajiunga Facebook unakosa mengi. Fanya haraka ujiunge na mtandao unaokupa nafasi ya kutafuta marafiki wapya sambamba na kuchati na wale waliomo kwenye orodha ya marafiki zako wa Facebook.
Pia unaweza kupenda hizi:
WhatsApp ni nini?
Nini maana ya mtandao wa kijamii?
Google Play Store ni nini?.
Nini maana ya simu za mkononi?
Facebook ni nini?
More Articles
Habari za michezo
Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017
Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC
Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup
Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe
Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup
No comments:
Post a Comment