Maana ya mtandao wa kijamii
Mtandao wa kijamii ni aina ya tovuti au aplikesheni inayowaruhusu watumiaji kuwasiliana kwa kuchapisha na kutumiana jumbe za maandishi, picha, video, kwa kutumia computer au simu za mkononi.
Mitandao ya kijamii huwaleta watu pamoja ambapo hujadili mada mbalimbali za kisiasa, kielimu, kiuchumi, kidini, n.k. Mitandao hii imerahisiha sana katika mawasiliano ambapo kwa muda mfupi sana mtu anaweza kusambaza ujumbe duniani kote.
Kila kukicha wataalam wa maswala ya teknolojia hubuni mbinu mpya na bora zaidi za kuwawezesha watu kupashana habari mbalimbali, na wataalam wanaotengeneza mitandao ya kijamii wanapaswa kushukuriwa sana kwa sababu bila mitandao ya kijamii tusingepata nafasi ya kupashana habari juu ya mambo mbalimbali yanayotokea ulimwenguni kote.
Leo hii hata wanasiasa wanafanya kampeni zao za uchaguzi kupitia mitandao ya kijamii, vilevile baada ya uchaguzi wanatoa mirejesho juu ya uwajibikaji wao kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii. Hata viongozi wa dini wanatumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kufikisha neno la Mungu kwa wanadam.
Baadhi ya mitandao ya kijamii ni Facebook, Pinterest, Twitter, WhatsApp, LinkedIn, Instagram pamoja na Google+. Mingine ni tango, Jamii Forums, BBM, Imo, Viber, Friendster, Myspace pamoja na StumbleUpon. Hiyo ni baadhi tu ya mitandao iliyojizolea umaarufu mkubwa.
Facebook ni mtandao unaongoza kwa kuwa na watumiaji wengi zaidi kuliko mitandao mingine. Mitandao mingine inayoonekana kutumiwa na watu wengi ni Twitter, WhatsApp pamoja na Google Plus (Google+).
Mitandao ya kijamii ina manufaa makubwa sana kwa wafanyabiashara, kwani inaruhusu wafanya biashara kutangaza bidhaa na huduma zao bure au kwa kiwango Fulani cha pesa, lakini mfanyabiashara akitoa pesa biashara yake huwafikia wateja wengi zaidi na kujikuta akiuza bidhaa au huduma kwa wingi.
Mitandao ya kijamii pia inamnufaisha mtumiaji wa kawaida kujipatia marafiki wapya kutoka sehemu mbalimbali wa kubadilishana nao mawazo juu ya maswala mbalimbali ya kimaisha.
Pia mitandao kama Facebook, huwaweka karibu watu waliosoma pamoja ambao kutokana na sababu mbalimbali wametengana kwa maana wanaishi katika maeneo tofauti ya kijiografia. Marafiki hao hukumbushana matukio mbalimbali waliyoyashuhudia pamoja kipindi cha nyuma, mathalani kipindi wakiwa masomoni au kipindi wakiishi mtaa mmoja.
Pamoja na faida nyingi za mitandao ya kijamii, tafiti zimeonyesha kuwa, kuna madhara katika utumiaji wake. Miongoni mwa madhara ya kutumia mitandao ya kijamii ni pmaoja na kuweka hadharani taarifa zako binafsi zikiwemo zile za faragha, kitendo ambacho kinaweza kukugharimu baadae hususan zikiangukia katika mikono mibaya (watu wabaya).
Madhara mengine ya utumiaji wa mitandao ya kijamii ni watumiaji kupoteza muda mwingi wakiwa kwenye mitandao ya kijamii wakichati na marafiki zao badala ya kutumia muda huo kujitafutia riziki zao au kujenga maisha yao.
Pia unaweza kupenda hizi:
WhatsApp ni nini?
Nini maana ya mtandao wa kijamii?
Google Play Store ni nini?.
Nini maana ya simu za mkononi?
Facebook ni nini?
More Articles
Habari za michezo
Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017
Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC
Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup
Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe
Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup
No comments:
Post a Comment