We Like Sharing

Monday, January 23, 2017

Google Play Store ni nini?

Google Play Store ni nini?

Google Play Store ni nini?

Google Play Store ni aplikesheni rasmi iliyotengezwa na kampuni ya Google Inc. kwa ajili ya kuwaruhusu watumiaji wa simu za mkononi zinazotumia Android OS, kupakua program bila malipo au kwa kulipia.

Applications zinazopatikana kupitia kwenye Play Store hutengenezwa au kuendelezwa na Google au waendelezaji wa tatu (Third-party developers), kila App ina matumizi tofauti japo kuna nyingine zinafanana kimatumizi.

Google Play Store ni njia ya pekee ya kupakua na kuingiza aplikesheni za APK kwenye simu zinazotumia Android Operating System bila kubadili mipangilio ya awali (default settings) kwa ajili ya kuruhusu kuingiza applications zinazotoka kwenye vyanzo visivyojulikana (unknown sources).

Kwa ajili ya kukabiliana na ueneaji wa program hatarishi (Malware), Google walitambulisha feature mpya ijulikanayo kama Bouncer mwaka 2012, ambayo inafanyakazi ya ku-scan Apps kabla ya kuruhusiwa kupakuliwa kupitia Play Store.

Mbali na kuruhusu kupakua Applications, Program ya Play Store inaruhusu pia kupakua Movies pamoja na michezo (Games) ya kwenye simu, ambapo mtumiaji wa andoid anaweza kupakua movie na kuitizama kwa kutumia simu, kompyuta au Televisheni yake.

Program hii ilianza kufanyakazi machi 2012, na mwanzoni ilijulikana kama Market store. Kupitia Google Play Store mtumiaji wa anaweza kupakua program za aina yoyote zinazopatikana kwenye program hiyo, almradi awe amejiunga kifurushi cha data au atumie Wi-fi na awe na akaunti ya Google Playstore kwenye smartphone au tablet yake.

Baadhi ya Apps unazoweza kupakua na kuingiza kwenye simu yako kupitia Google Play store ni pamoja na Facebook, Chrome, Opera Mini, WhatsApp, Camera 360, Youtube, Instagram, Imo, viber na Media Players. Nyingine ni File Manager, Gallery, E-mail Apps, facebook Messenger pamoja na Google Drive.

Pia unaweza kupenda hizi:

WhatsApp ni nini?
Nini maana ya mtandao wa kijamii?
Google Play Store ni nini?.
Nini maana ya simu za mkononi?
Facebook ni nini?

Related Articles

Kulazimisha simu isome 3G tu

4G LTE ni nini?

3G ni nini na inafanyaje kazi?

2G ni nini na inafanyaje kazi?

Internet Configurations za Airtel

Internet Configurations za Halotel

Habari za michezo

Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017

Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC

Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup

Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe

Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment