Vituko vya wanafunzi mashuleni!
Mwalimu aliingia darasani na mazungumzo kati yake na wanafunzi wake yalikuwa kama ifuatavyo:
Mwalimu:
Atakayefanikiwa kujibu vizuri swali nitamruhusu aende nyumbani
Mwanafunzi_1:
Vuuuuu...Puuuu(mwanafunzi akarusha begi lake nje kupitia dirishani).
Mwalimu:
Nani karusha begi nje?
Mwanafunzi_1:
Mimi
Mwalimu:
Kwanini?
Mwanafunzi_1:
Kwa sababu nilijua utaniuliza swali rahisi, kwa hiyo niliamua kurusha kabisa begi langu nje, ili nikimaliza kujibu niweze kutimka faster, na tayari nimeshajibu swali lako, kwa hiyo naondoka, kwa heri mwalimu!
Mwalimu:
Panzi wee kuja hapa nikutie adabu nyang'au wee...
Vichekesho na Chemsha bongo zaidi...
Tukio lililoweza kusababisha ugomvi!
Tuchukulie imekutokea wewe, utachukua uamuzi gani?
Je, wewe Ungerudisha Au Ungemalizia?
Vituko vya wanafunzi mashuleni!
Mwanafunzi huyu anachekesha kwa vituko vyake!
Dogo janja atibua mipango ya michepuko!
Binti amjaza hasira mama yake!
Nani atagundua hiyo rangi moja?
Chambo ya nini kwa samaki aliyevuliwa?
Kati ya mke na mume nani muongo zaidi?
No comments:
Post a Comment