Chambo ya nini kwa samaki aliyevuliwa?
Mwanaume na mwanamke walikuwa wanapendana sana kabla ya ndoa. Mara kwa mara mwanaume alikuwa anampa zawadi za kila aina mpenzi wake, kitu kilichopelekea mwanamke ajione wa kipekee sana na anapendwa sana na jamaa.
Baada ya kuoana, mwanaume alisitisha mazoea ya kununua zawadi kwa ajili ya mkewe. Siku moja mkewe aliamua kuvunja ukimya wake kama ifuatavyo:
Mke:
Mume wangu!
Mume:
Naam mke wangu...
Mke:
Kabla hatujaoana ulikuwa unaninunulia zawadi na vitu kibao vya gharama.
Mume:
Ndiyo...! Kwa hiyo?
Mke:
Kwanini siku hizi hufanyi hivyo?
Mume:
Hivi umewahi kumuona mvuvi anayempa samaki chambo baada ya kumvua?
Mke:
Mmmmmmhhh
Vichekesho na Chemsha bongo zaidi...
Tukio lililoweza kusababisha ugomvi!
Tuchukulie imekutokea wewe, utachukua uamuzi gani?
Je, wewe Ungerudisha Au Ungemalizia?
Vituko vya wanafunzi mashuleni!
Mwanafunzi huyu anachekesha kwa vituko vyake!
Dogo janja atibua mipango ya michepuko!
Binti amjaza hasira mama yake!
Nani atagundua hiyo rangi moja?
Chambo ya nini kwa samaki aliyevuliwa?
Kati ya mke na mume nani muongo zaidi?
No comments:
Post a Comment