We Like Sharing

Monday, November 30, 2015

Mwanafunzi huyu anachekesha kwa vituko vyake

Mwanafunzi huyu anachekesha kwa vituko vyake

Mwanafunzi huyu anachekesha kwa vituko vyake!

Mwalimu wa somo la kiingereza aliingia darasani na kuwaambia wanafunzi wamtajie mnyama mwenye jina linaloanzia E. Wanafunzi wote wakanyoosha mikono.

Wakati mwalimu anatafuta mwanafunzi atakayemchagua kujibu swali, mwanafunzi mmoja akapiga kelele akisema - Elephant. Mwalimu akampongeza mwanafunzi huyo kwa kupatia jibu, ila alikereka kwa kitendo cha mwanafunzi huyo kujibu swali wakati hakuchaguliwa.

Mwalimu akawaambia wanafunzi wataje jina la mnyama linaloanza na herufi T, mwanafunzi yule yule akasikika akisema Two Elephants.

Mwalimu alikasirika na kuamua kumtoa nje mwanafunzi huyo. Baada ya hapo akawaambia tena wanafunzi wamtajie jina la mnyama linaloanza na herufi M. Sauti ileile ya mwanafunzi yule aliyetolewa nje ikasikika kupitia dirishani - Maybe an Elephant...

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment