Rais mteule wa Gambia, aapishwa nje ya nchi
GambiaRais mteule wa Gambia aliyeshinda uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi desemba 2016 nchini humo katika nafasi ya urais, alilazimika kuapishwa katika ofisi za ubalozi wa Gambia nchini Senegal.
Hiyo ilikuja kutokana na mteule huyo kuhofia usalama wake baada ya mpinzani wake, Yahya Jammeh, kung’ang’ania madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi huo, ambapo Jammeh anapinga matokeo ya uchaguzi kwa madai kuwa uchaguzi haukufuata taratibu.
Akila kiapo cha utii, Adama Barrow alitoa wito kwa wanajeshi kuonesha utii kwa serikali yake pindi atakapoingia ikulu. Barrow ameungwa mkono na jumuiya ya kimataifa, huku mpinzani wake, Jammeh akipinga vikali kuondoka madarakani huku akishinikiza pingamizi lake lisikilizwe kwanza.
Awali, Rais Yahya Jammeh, ambaye amekikalia kiti cha urais nchini humo kwa takribani miaka 22, alikubali matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na tume ya Uchaguzi, lakini baada ya siku kadhaa aliyakataa na kwenda mahakamani kushtaki akidai kuwa matokeo hayakuwa sawa.
Kwa upande mwingine baadhi ya watumishi kadhaa wa tume ya uchaguzi nchini humo wamekimbilia nchi jirani hususan Senegal baada ya kusikia tetesi kuwa serikali ya Jammeh ilikuwa inataka kuwatia nguvuni kutokana na kumtangaza Barrow kuwa mshindi wa uchaguzi dhidi ya jammeh.
Wengine wanasoma hizi:
Habari za michezo
Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017
Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC
Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup
Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe
Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup
No comments:
Post a Comment