We Like Sharing

Saturday, January 21, 2017

Rais Yahya Jammeh aachia madaraka ya Urais Gambia

Rais Yahya Jammeh aachia madaraka ya Urais Gambia

Rais Yahya Jammeh aachia madaraka ya Urais Gambia

Gambia

Aliyekuwa Rais wa Gambia na aliyeng'ang'ania madarakani baada ya kucshindwa katika uchaguzi mkuu nchini Gambia, Yahya Jammeh, leo amekubali kuachia madaraka ya kiti cha urais nchini humo. Hii inatokana na shinikizo kutoka kwa marais wa mataifa ya magharibi mwa Afrika yanayounda jumuiya ya kiuchumi inayojulikana kama ECOWAS (Economic Community of West African States).

Taarifa hizo zimethibitishwa na mgombea aliyeshinda katika uchaguzi huo, ambaye jioni ya tarehe 20/1/2017 aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa Jammeh ameachia ngazi ya urais na ametoweka nchini humo na bado haijawekwa wazi alikoelekea.

"Napenda kuwajulisha kuwa Yahya Jammeh ameachia madaraka na ametoweka nchini". Aliandika Adama Barrow kwenye chapisho lake la kwenye Twitter.

Adama Barrow alikimbilia nchini Senegal baada ya uchaguzi kutokana na Rais Jammeh kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita (disemba 2016) na kung'ang'ania madarakani. Kilichomtia hofu zaidi hadi akaamua kwenda kujihifadhi nchini senegal, ni tetesi zilizokuwa zinadai kuwa Rais Jammeh alikuwa anaandaa mpango wa kumfunga jela Barrow.

Rais Yahya Jammeh alikaa madarakani kwa muda wa miaka 22, na baada ya kushindwa kwenye uchaguzi uliopita alitaka kuendelea kukikalia kiti cha urais nchini humo, kitendo kilichoonesha kutowafurahisha wengi wakiwemo Umoja wa Kimataifa pamoja na mataifa ya Afrika magharibi.

Kutokana na Rais Jammeh kukataa kutoka madarakani, viongozi wa nchi jirani waliamua kuingilia kati kwa ajili ya kusuluhisha mgogoro huo, ambapo lakini alioonekana kutokukubali kitendo kilichoyafanya mataifa yanayounda umoja wa ECOWAS kutuma majeshi yake nchini Gambia kwa ajili ya kumuondoa Jammeh ikulu kwa nguvu.

Mazungumzo yaliyofanyika leo ijumaa, baina ya Rais Jammeh na Rais Alpha Conde wa Guinea na Rais Mohamed Ould Abdel Aziz wa Mauritania, yalileta mwafaka wa mgogoro huo kwa Rais Jammeh kuachia kiti cha Urais na kutoweka nchini humo.

Wengine wanasoma hizi:

Jinsi ya kuweka screen lock kwenye android

Kampuni kubwa zinazotengeneza Smartphones

Rais mteule wa Gambia, aapishwa nje ya nchi

Mambo ya kufanya baada ya kununua smartphone

Habari za michezo

Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017

Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC

Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup

Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe

Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment